VILIO na simanzi vimetawala katika wilaya za Tanga Mjini na Muheza mkoani Tanga, baada ya nyumba za wananchi, zikiwemo za makazi na biashara, kupigwa alama ya X na Shirika Hodhi la Reli (Rahco) kwa ajili ya kubomoa kwa madai ya kujengwa ndani ya eneo la hifadhi ya njia ya treni.
Nyumba za biashara, yakiwemo maghorofa, zimedaiwa kuwa ndani ya mita eneo la hifadhi ya reli na kutakiwa kubomolewa kabla ya mwezi Oktoba.
Zoezi la uwekaji X nyumba lilianza juzi Tanga na kufika jana wilayani Muheza katika kata ya Genge.
Maafisa hao wa shirika hodhi waliendesha zoezi hilo wakiwa na ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki na kuagiza wakazi hao wawe wamebomoa wenyewe nyumba zao ndani ya siku 30.
Maafisa hao walikuwa wakipima urefu wa mita 100 kutoka relini kila upande kuwa ndiyo eneo la hifadhi lakini katika baadhi ya maeneo upana huo ulifika mita 200.
Reli ya Korogwe-Muheza-Tanga, ambayo ni tawi la reli ya Dar es Salaam-Arusha, haijafanya kazi kwa miaka mingi hivyo wananchi wengi kujikuta wameisogelea kwa karibu.
Akizungumza na Nipashe, Joseph Ruwa, mkazi wa kijiji cha Genge ambaye nyumba yake ni moja kati ya zilizowekwa alama hiyo, alisema yeye na wenzake hawakubaliani na hatua hiyo kwa sababu walitangaziwa kwamba hifadhi ya reli mwisho ni mita 100.
Alisema wakazi wengi, akiwemo yeye ambaye ni mstaafu, wapo nje ya mita 100 lakini cha kushangaza wanaambiwa hifadhi ni mita 200.
Alisema maafisa hao wa Rahco walifika na kuweka alama hiyo katika majengo bila ya kuwataarifu wenye nyumba.
Wananchi 4,000 wanaoishi kitongoji cha Majani Mapana, kata ya Tanganyika wilayani Muheza mkoani Tanga waliandikiwa barua ya kubomoa nyumba zao na Rahco mwezi uliopita.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Muheza, Peter Jambele alisema anataka kwanza kujidhirisha ni nyumba ngapi zimejengwa ndani ya hifadhi ya reli ili zitakapobomolewa wenye nyumba watafutiwe viwanja vingine.
Chanzo:Nipashe

No comments:
Post a Comment