Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart akiwa na Mkuu Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.
Uingereza imetoa msaada wa dola za Marekani Milioni 450 sawa na takribani shilingi Trilioni 1 za Tanzania kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
Msaada huo umetangazwa leo tarehe 23 Agosti,2017 na Waziri wa Nchi anayeshughulikia maendeleo ya Kimataifa na masuala ya Afrika katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola ya Uingereza Mh.Rory Stewart muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar
No comments:
Post a Comment