KIUNO kuuma ni tatizo la kiafya na ni moja ya mambo ambayo yanasababisha idadi kubwa ya watu kwenda mahospitali eidha kulazwa au kuhudhuria kliniki kutibiwa.
Maumivu ya mgongo au kitaalamu lumbago yana uhusiano mkubwa sana na misuli na mifupa. Ni vyema kwanza tukaangalia mfumo wa mgongo wa mwanadamu ambao kitaalamu huitwa vertebrae.
Sehemu ya juu eneo la shingo linaitwa cervical spine, sehemu ya mabega na chini yake huitwa thoracic na sehem ya chini ya mpaka makalio yanapoanzia huitwa lumber. Ukishuka chini kidogo kuanzia makalio yanapoanzia seheme ya chini yenye mwonekano kama mkia huitwa coccyx.
Maumivu ya kiuno yanaweza sababishwa na matatizo kwenye nyonga kitaalamu sacroiliac au misuli hali ambayo huitwa lumbago.
Mifumo ya fahamu nayo haswa ya sciatica nerve (eidha neuralgia au neuritis) hali hii huanza kusikika pale ambapo kutakuwa na kuguswa au kuathiriwa na kitu chochote. Hali hiyo husababisha mawasiliano kukatika kati ya ubongo na miguu na matokeo yake ni mtu kuwa mlemavu yaani kushindwa kunyanyua mguu au kuusogeza.
VYANZO
Katika pingili yaani vertebral disc maumivu yanatokea pale ambapo kutakuwa na kupasuka au kulika kwa gegedu zinazounda pingili za kiuno. Misuli dhaifu na tindikali nyingi inayoingia kwenye damu pamoja na upungufu wa madini ya chokaa hali huwa mbaya zaidi.
Kuharibika kwa misuli eneo husika, mifupa na kano kitaalamu ligament, figo na kibofu cha mkojo, matatizo ya tezi dume au kizazi kwa akina mama ni sababu za mtu kuumwa mgongo.
Misuli iliojishikiza kwenye kiuno huathiriwa na tabia mbaya ya ulaji na uvaaji usiozingatia kanuni za afya bila kusahau magonjwa ya mifupa yaani arthriti.
No comments:
Post a Comment