Bi. Grace Mugabe ambaye ni mke wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ajisalimisha katika kituo cha Polisi nchini Afrika Kusini, baada ya tuhuma za kumpiga binti ambaye alimkuta na mwanaye wa kiume hotelini.
Grace Mugabe alimpiga binti aliyejulikana kwa jina la Gabriella Engels (20) ambaye ni mwanamitindo na kamba ya 'cable', baada ya kumkuta hotelini na watoto wake wa kiume Robert Mugabe Jr (25) na Chatunga Mugabe( 21)
Waziri wa Jeshi la Polisi wa Afrika Kusini aliviambia vyombo vya habari kuwa anatarajia kupokea ripoti rasmi ya uchunguzi wa tukio hilo, na ndipo sheria ifuate.
Vyombo vya habari kutoka Afrika Kusini vimeripoti kuwa Bi. Grace Mugabe atawasili Mahakamani muda wowote kuanzia sasa, na taarifa kamili ya kinachoendelea bado haijawekwa wazi.
No comments:
Post a Comment