MWENYEKITI wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani. Mwenyekiti huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.
Pamoja na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor.













No comments:
Post a Comment