KUTOKANA na mwitikio mkubwa wa ulipaji kodi za majengo, uliosababisha benki kufurika wateja katika siku ya mwisho ya kulipa kodi hiyo, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), imelazimika kuongeza siku 14 zaidi na kwamba baada ya hapo, malipo yatakwenda sambamba na adhabu.
Kuongezwa kwa siku hizo, kumethibitishwa na TRA katika taarifa yake kwa umma, ikisema muda wa kulipa kodi ya majengo kwa mwaka 2016/2017 bila adhabu umeongezwa hadi Julai 15, mwaka huu. “Baada ya hapo kodi hiyo italipwa na adhabu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Serikali, kuanzia mwaka wa 2016/2017 imeanzisha kodi ya majengo kwa wamiliki wote wa nyumba, kiasi cha chini katika maeneo mengi, hasa yasiyothaminiwa kikiwa Sh 10,000. Hata hivyo, kodi hizo hazigusi nyumba za vijijini, zilizojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi, kwa maana ya zisizo za kudumu.
No comments:
Post a Comment