Nikiwa na miaka 17, nikipata mshahara wangu wa kwanza kama mcheza soka, nilijenga nyumba kwa ajili ya ndugu zangu na kuhakikisha wako salama. Kama nyote mjuavyo, nilipokea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Nilimpandisha mama yangu jukwaani kumshukuru kwa kila kitu. Mwaka huo huo nikampeleka Uingereza (London) kwa ajili ya kukagua afya yake.
Binti yangu alipozaliwa, tuliwasiliana na mama yangu kumpa habari hizo njema lakini palepale akakata simu na kutotaka kusikiliza habari hiyo. Nilimpa mama kiasi kikubwa cha fedha kuanzisha biashara ya mapishi na masuala mengine.
Nikawaomba ndugu zangu waweke picha yangu na jina langu kwenye bidhaa na huduma hizo ili waweze kuuza zaidi. Ni kitu gani kingine kijana anaweza kukifanya kuisaidia familia yake?
Ndugu zangu wamenifanyia mambo mengi sana yasiyopendeza, nilifanya kila niwezalo kubakia Real Madrid lakini kwa sababu ya Marehemu Kaka yangu sikuweza kubakia pale, alituma barua rasmi kwenye Klabu kutoka kwa familia yetu na kuitaka klabu isiendelee kunibakisha Madrid. Sisemi kwamba hiyo ndiyo sababu iliyofanya waniache niende, lakini inaweza kuwa ilichangia hata kama ni asilimia 10.
Leo nayaona maisha kwa namna tofauti kabisa. Mama yangu anasema sijawahi kumpa hata dola 200, Watu hawajui kuwa nimenunua nyumba kadhaa kwa ajili ya ndugu zangu, nimenunua magari kwa ajili ya ndugu zangu kwa hiyo nasikitika kuwa mama yangu na ndugu zangu wanasema mambo kama haya!
Mama yangu alinipa fursa ya kuwa mimi leo hii, na hakuna ntakachofanya kumshukuru kwa upendo wake kwangu. Namshukuru kwa kuwa mama yangu, namshukuru kwa kuwa na mimi kwenye nyakati ngumu, lakini leo mimi ni Adebayor, na napaswa kuwasaidia watu wengine pia.
Kwa sasa sizungumzi na familia yangu tena lakini nazungumza na marafiki zangu. Niko tayari kuzungumza na yoyote kwa sababu mimi ni muumini mzuri, lakini mimi na familia yangu tumepitia mambo mengi na ukweli ni kuwa ndugu zangu na mama yangu hawanisaidii kufanya kazi yangu vizuri.
Mara nyingi sana nimepata majeraha kwenye mechi, mama yangu na ndugu zangu hawajawahi kunipigia kunijulia hali. Ikitokea wananipigia simu ni kuomba kitu. “Nijali ili na mimi nikujali, Usijali pesa zangu tu na akaunti zangu, mwisho wa siku unasema damu ni nzito kuliko maji, kwa nini unasahau damu yangu na unakumbuka pesa zangu?”
Lakini mimi nimeamua kuchagua furaha binafsi (peace of mind) na siku zote nina furaha!
No comments:
Post a Comment