Serikali imesimamisha utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini hadi Tume ya Madini itakapoundwa na kuanza kazi na kwamba kwa sasa baadhi ya shughuli zitakazofanywa na tume hiyo zitafanywa chini ya usimamizi wa Kamishna wa Madini.
Hatua hiyo inatokana na uwepo wa Sheria mpya iliyoanza kutumika Julai 7, mwaka huu ambayo pia imeufuta Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, James Mdoe ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mbali na kufutwa kwa wakala huo pia sheria hiyo imeelekeza kuanzishwa kwa tume ya madini, kuongeza malipo ya mrabaha kutoka asilimia nne kwa madini ya Metali (dhahabu, shaba, fedha) hadi asilimia sita.
Pia imeelekeza kuongezeka kwa malipo ya mrabaha kutoka asilimia 5 kwa madini ya almasi na vito hadi asilimia sita
No comments:
Post a Comment