Wednesday, 12 July 2017

KUAGWA KWA MAREHEMU ‘BIKIRA WA KISUKUMA’ VIWANJA VYA LEADERS, DAR



Jeneza la mwili wa marehemu Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’ likiwa viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuombewa na kuagwa leo jijini Dar es Salaam.


Ndugu na jamaa wakiwa katika shughuli ya kumuaga marehemu.

Umati ukiwa katika viwanja vya Leaders tayari kwa kumuombea na kumuaga marehemu Seth. Pembeni kulia ni kibao kinachoonyesha kipindi cha ‘Ubaoni’ alichokuwa anatangaza marehemu Seth kituo cha Radio cha Efm.

Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio.

Meneja Mkuu wa Efm Radio na TV-E, Dennis Ssebo (mbele) akitafakari jambo mbele ya jeneza la marehemu (halipo pichani)

Baba wa marehemu, Mzee Katende (wa tatu kushoto) akiwa na jamaa wa familia yake.

Mkurugenzi wa Efm Radio na TV-E, Francis Ciza aka Majizo (aliyeinama, T-shirt nyeusi) akitafakari jambo.
MWILI wa marehemu Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, kipindi cha Ubaoni, umeagwa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, safari ya kuelekea kwenye makazi yake ya milele, kwenye Makaburi ya Kinondoni ilianza ambapo hatimaye maziko yamefanyika mchana wa Juni 12, 2017.
Bikira wa Kisukuma, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.
Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!