Leo tarehe 28 July ni Siku ya Homa ya Ini Duniani. Ugonjwa wa Homa ya Ini ni Tatizo linalohitaji juhudi za pamoja za kupambana nao.
Ugonjwa huu umetajwa kuwa wa hatari na unaoua idadi kubwa ya watu polepole. Kati ya watu 100, watu 8 wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huu na wanaweza wasionyeshe dalili.
– kwa Tanzania, takwimu chache zilizopo zinaonyesha uwepo wa Maambukizi ya Virusi vya Hepatitis B na C. Mfano kati ya wachangiaji damu 200,000 asilimia 6 kati yao walikuwa na maambukizi ya Hepatitis B
– Kila mtu achukue hatua kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.
– Chanjo ya ugonjwa huu hutolewa kwa mtu asiye na maambukizi ya kirusi. Hapa nchini kuanzia mwaka 2003, chanjo dhidi ya Hepatitis B hutolewa kwa watoto wachanga waliozaliwa kuanzia mwaka 2003 ambayo ipo kwenye mchanganyiko wa Chanjo ya Pentavalenti. Hadi sasa, Takribani asilimia 97 ya watoto wamepata chanjo hii.

– Mwelekeo wa Serikali ni kuendelea kutoa chanjo dhidi ya Hepatitis B kwa watoto wachanga wote nchini na pia kuhakikisha chanjo hii sasa (ya Hepatitis B) inapatikana kwa watu wengine wote watakaohitaji na kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment