Wednesday, 26 July 2017
JPM-“Nikiondoka Hakuna Atakayekuwa Kama Mimi”
Rais Magufuli leo July 25, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alikuwa katika Mkoa wa Singida alikozindua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa km 89.3 ambapo mbali na kufanya uzinduzi huo alipata nafasi ya kuhutubia wananchi.
'Pengine nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja baada ya mimi' - Rais @MagufuliJP
'Ni lazima niyatapike yote haya, nikikaa nayo nitapata presha bure, ila wale walioyafanya wakumbuke na madhambi yao' - Rais @MagufuliJP
'Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo lakini pia siwezi nikaacha kusema' - Rais @MagufuliJP
'Nataka Tanzania hii iwe kama Ulaya na tutafika tu, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kweli kweli'- Rais @MagufuliJP
'Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao'- Rais @MagufuliJP
'Niliporudishwa wizara ya ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha' - @MagufuliJP
Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo Dar es salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua - Rais @MagufuliJP
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment