Wednesday, 26 July 2017

JPM: Hakuna chakula kwa mkoa au wilaya itakayokumbwa na baa la njaa

Image may contain: mountain, sky, plant, grass, outdoor and nature
Rais John Magufuli amesema Serikali haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa na baa la njaa na badala yake viongozi wa mkoa huo watawajibishwa.

“Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,” amesema.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Itigi, Mkoani Singida baada ya kufungua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye kilomita 89.3 na kumaliza ziara yake katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida.
“Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,” amesema.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kusisitiza kuwa Serikali haitajishughulisha na Mkoa au Wilaya ambayo itakumbwa na njaa na kusisitiza wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kuepukana na hali hiyo.
Hatahivyo, baadhi ya wanasiasa kutoka upinzani wamekuwa wakidai kuwa ni jukumu la Serikali kusaidia watu pale wanapokumbwa na majanga ikiwemo baa la njaa



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!