MKAZI wa Mtaa wa Tambukareli, Manispaa ya Shinyanga, Sarah Bundala (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake baada ya kushindwa kufanya marejesho ya mkopo aliokuwa amemdhamini rafi ki yake aliyetoroka na pesa, ingawa haijafahamika ni kiasi gani.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, Jumanne Muliro amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo la juzi majira ya saa 10:00 jioni. Kabla ya kujinyonga, mama huyo alikuwa na rafiki yake wakihangaika pamoja kutafuta pesa ili apate za kupeleka kwenye marejesho ya mkopo ambao alikuwa amemdhamini rafiki yake aliyetoroka kusikojulikana.
Akielezea tukio hilo, rafiki yake wa karibu Mariamu Mugaya, alisema majira ya saa 8:00 mchana alimwita ili amsindikize kutafuta pesa za kurudisha mkopo, lakini walizunguka bila mafanikio, ndipo akamshauri ampigie simu mumewe amsaidie kiasi hicho cha pesa anachohitaji, lakini akagoma kufanya hivyo.
Baada ya kushauriana mahala pa kupata pesa, lakini wakazikosa, marehemu alimwambia aenda nyumbani, ili yeye akalale kwanza na ikifika majira ya saa 10:00 jioni arudi kumuona na kwamba hata watu wakimuuliza yuko wapi, awaambie amelala nyumbani kwake asiwafiche. Lakini ilipofika muda huo, akapokea taarifa ya kujinyonga kwa rafiki yake.
No comments:
Post a Comment