Saturday, 29 July 2017
73 wadakwa kwenye msako wa wizi wa magari na vifaa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Lucas Mondya ikiwa ni miezi kadhaa toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo.
Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya alisema katika opesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pump, starter na seat cover.
“Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73 tunawashikilia, Kinondani wamekamatwa watuhumiwa 29, Ilala wamekamatwa wahutumiwa 33 na mkoa wa kipolisi Temeke wamekamatwa wahumiwa 11,”
Alisema jumla ya power windows zilizokamatwa ni 40, Raidio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya magari 109, wiper switch 7, Tampa 4, left pump3, Air cleaner 1, Booster 3, show grill 6, machine za kupandisha vino 1 na tyre used 2.
Pia alisema katika mahojiano na wahutumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni namna gani na wapi wamevipata.
Wahutumiwa wote bado wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahamani kwa hatua zaidi.
Kwa upande wa RC Makonda alisema yeye anataka kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa salama ili kutimiza shauku ya Rais John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment