Monday 5 June 2017

Yanayojiri Viwanja vya Majengo Moshi Kuaga Mwili wa Mzee Ndesamburo

MOSHI: Shughuli ya kuuaga mwili wa mmoja wa waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na siasa za mageuzi Mzee Philemon Ndesamburo imeanza katika Viwanja vya Majengo, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mzee Ndesamburo ni mmoja ya waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa miaka 15 na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwili waMzee Ndesamburo ukietolewa Mochwari ulipokua umeifadhiwa na kuelekea Uwanja wa Majengo kwa ajili ya kuuaga kabla ya kuzikwa.
Mzee Ndesamburo alifariki dunia wiki iliyopita Mei 31, 2017 baada ya kuzidiwa ghafla ofisini kwake na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa KCMC.
Jeneza lenye mwili wa marehemu mzee Ndesamburo
Taarifa zilieelea kuwa, Mzee Ndesamburo alikuwa ofisini kwake akimwandikia cheki ya benki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro kwa ajili ya kutoa rambirambi ya vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi, Lucky Vincent, Karatu ambapo kabla hajamalizia kuandika, hali yake ilibadilika ghafla. Meya aliamchukua na kumkimbiza hospitali ambapo kabla ya kuanza kutibiwa alipoteza maisha.






















PICHA KWA HISANI YA GPL.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!