Wednesday, 7 June 2017

Mwingine apigwa risasi mchana huu Mkuranga

No automatic alt text available.
Habari za hivi punde, zinaeleza kwamba mtu mwingine amepigwa risasi katika Kijiji cha Songa, Mkuranga majira ya saa tisa mchana wa leo (June 7, 2017).

Tukio hilo limetokea saa chache baada ya IGP Simon Sirro kuzuru ukanda huo unaoongoza kwa mauaji ya raia yenye utata. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha mtu huyo kupigwa risasi lakini akasema anayeweza kuthibitisha kama amekufa au laa, ni daktari lakini taarifa alizonazo yeye ni kwamba amejeruhiwa kwa risasi. 

Mtu mwingine, Eric Mwarabu ambaye alikuwa ni askari mgambo, jana usiku alipigwa risasi na kuuawa akiwa nyumbani kwake. Mwenye taarifa zaidi azidi kutujuza.


CHANZO:JMF

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!