Thursday, 8 June 2017

MFUMO BORA WA MAISHA KWA AFYA BORA

Image result for mazoezi

Mfumo wa maisha wa mwanadamu unatakiwa kuwa bora ili awe na afya bora,afya nzuri hailetwi kwa lishe tu ,inachangia na  lifestyle yako. Lazima uwe na mpangilio ulio mzuri kuanzia unapoinza siku asubauhi yako mpaka unaporudi kulala usiku.


Afya nzuri inajengwa na lishe na mazoezi ,binadamu unatakiwa uwe makini kwenye vitu vifutavyo iwapo utafatilia utaishi kwa afya nzuri


Kunywa maji ya kutosha-binadamu unatakiwa kunywa maji glasi 8 kwa siku ,hilo unatakiwa ulizingatie na wanao ishi maeneo ya joto sana wanaweza kunywa zaid ya hayo,maji yakusafisha mwili kutoa sumu,maji hayo hayo yatakufanya kuwa na ngozi laini ,kulainisha choo ,maji yana faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu hivyo ni muhimu kuzingatia hilo.


Jipe muda wa kulala-binadamu anatakiwa kulala masaa 8 kwa siku hivyo nivizuri kupumzisha mwili na akili itakusaidia kuwa na kumbukumbu ya kutosha,kukuepusha na kiharusi,kukusaidia kunenepa,

Kula matunda na mboga za majani za kutosha-zinakupa virutubisho vya kutosha,kukukinga na maradhi,kusaidia kupata choo kwa urahisi kwa wale wenye tatizo la constipation,kusaidia kuwa na ngozi laini ,kuweza kuona vizuri (kuimarisha macho) na faida nyinginezo nyingi.


Mazoezi-binadamu tunatakiwa kufanya mazoezi ya miili yetu ili kuikinga na maradhi,kupunguza uzito,kutoa mafuta na sumu tunayoila kupitia vyakula,mazoezi muhimu kwa mama mjamzito,watu wenye pressure, uzito mkubwa, na maradhi mengine sugu ,mazoezi yapo ay aina nyingi unaweza kwenda gym,au ukafanya nyumbani ya kukimbi,kuruka kamba,kuogelea,kutembe mwendo mrefu,kuendesha baiskeli,kucheza mziki  na mengineo mengi irimradi mwili wako uwe na movements nyingi.

Epuka kula vyakula visivyo na virutubisho-proccessed foods kawaida zinakuwa sio fresh vinakuwa na chemicals na sukari kwa wingi,acha kula vyakula vya kukaangwa vinatumia mafuta mengi na yana calories nyingi itakayo kuletea unene au matatizo ya moyo.

  • Epuka sukari nyingi -kula vitu vya sukari sio vizuri kwa afya yako utaongezeka uzito kwa haraka,utaoza meno n.k. Kama ulaji ya ice cream,chocolate ,pipi  n.k sio mzuri kwa afya yako.

  • Positive mental health-kaa na watu wenye mawazo chanya sio hasi ,watu wenye mawazo chanya wanafaida kwako na afya yako hawata kupa stress ila watu wenye mawazo hasi watakufanya uwe na msongo wa mawazo wao wanawaza kumsema mtu vibaya au kufanya matendo mbaya .



  • Jiamini-unatakiwa kujiamini kwa kila ufanyalo kwani usipo jiamini utapata msongo wa mawazo na hapo utahadhiri afya yako kwa namna moja au nyingine.

  • Zingatia size ya mwili wako-hutakiwi kuwa mnene wala mwembamba kuwa size ya kawaida kulingana na urefu wako ,uzito mkubwa au uzito mdogo sana ni madhara kwa afya yako.


  • Epuka pombe na sigara-vinahadhiri afya yako kwa kiwango kukibwa kuadhiri maini,mapafu au figo n.k  ,na ni gharama kubwa unatumia kununua na kwa wakati huo huo unaboamoa afya kwa pesa yako.

Epuka kula bila kuhisi njaa-ni makosa kula wakati tumbo limejaa hapo unajaza tumbo 


  • Kula mapema-zingatia ratiba ya mlo kama asubuhi ni sa 2-3,chakula cha mchana ni  saa 6-7,usiku ni 12 jioni mpaka saa 2 usiku binadamu anatakiwa kula chakula cha usiku masaa 3 kabla ajalala kiafya chakula kinatakiwa kusagwa ukiwa ujalala,pili kula usiku sana kunasababisha kunenepa.


  • Usafi wa mwili wako- ujali mwili wako uwe safi kwa kuoga,kupiga mswaki,kunyoa nywele zisizo hitajika sehemu za mwili wako.


  • Usafi wa mazingira unayoishi -yanatakiwa kuwa masafi unapolala,kupika,kuoga n.k itakuepusha na maradhi haswa ya mlipuko.

Kutana na marafiki kubadilishana mawazo-unahitaji kutoka nje baada ya kazi au week end nenda kutana na marafiki mbadilishane mawazo kama mnavikundi vya maendeleo au umoja wa kikundi cha kidini ,upate habari mpya muhimu kwako ,nenda beach au cinema,kacheze tennis,bowling,mpira au nenda shopping,fanya kitu ambayo hufanyi mara kwa mara kurelax maind yako.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!