Saturday, 3 June 2017

CCBRT, TIGO TANZANIA WAUNGANA KUTIBU UGONJWA WA MIGUU PINDE KWA WATOTO

Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Sylvia Balwire akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Erwin Telemans, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.


 Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Erwin Telemans akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya  hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa  hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika  mapema leo jijini Dar es Salaam.



Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Sylvia Balwire akihutubia wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya  hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa  hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika  mapema leo jijini Dar es Salaam.



Mama mwenye mtoto  mwenye ugonjwa wa miguu pinde akizungumza na vyoombo vya habari mara baada ya makabidhiano ya  hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa  hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika  mapema leo jijini Dar es Salaam.


2 Juni 2017, Dar es Salaam: CCBRT imejikita  kutoa huduma za tiba zinazofikiwa na wagonjwa  wanazimudu, tiba vora na hali kadhalika kuzia  ulemavu na kukuza kujumuishwa kwake nchini Tanzania. Moja ya tukio kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kukuza  uelewa kuhusu  umuhimu wa kutambua mapema, kutafuta tiba na  na kufuatilia tiba yote ya miguu iliyopinda.
Mguu uliopinda ni ulemavu unaosababisha  ama mguu mmoja ay miguu yote kupinda. Mguu unaoathirika  unasababisha sehemu ya unyayo kubinuka kuelekea ndani kuanzia katika kifundo  au kutembelea pande za miguu badala ya unyayo. Hata hivyo utambuzi wa mapema pamoja na tiba katika umri mdogo, huwafanya watoto waliozaliwa na  na mguu uliopinda  kuweza kutembea  na kushiriki ipasavyo  katika shughuli za kijamii na kiuchumi  ndani ya jamii zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Usimamizi wa masuala ya Kiserikali wa Tigo, Sylvia Balwire alisema kuwa Tigo imejikita kurudisha kwa jamii ambamo inaendesha shughuli zake  kupitia mikakati wake wa kuwajibika kwa jamii. “Tuliona kuna haja ya kusaidia katika hili kwa sababu CCBRT inahudumia maskini walioko pembezoni ndani ya jamii na  inajaribu kuondoa vikwazo vingi kadiri iwezekanavyo  ili kuwawezesha watu kutafuta tiba. Jamii itaikumbuka CCBRT daima  kutokanana mkakati wake huu wa kuwasaidia watu walio na ulemavu na kuwapatia fursa ya kutibiwa kwa gharama nafuu. Inatakiwa mtu kuwa na moyo wa ziada  kutoa huduma ambayo CCBRT inatoa kwa jamii.

Zaidi ya watoto 1,509 walishanufaika na upasuaji huu unaobadili maisha  kutoka CCBRT katika kipindi cha zaidi ya miaka sita iliyopita. Haya ni mafanikio ambayo yanatufanya sisi sote tuliopo Tigo tunajivuania sana. Kupitia matibabu ya watu wanaoishi na ulemavu, Tigo na CCBRT wanaweka chapa ya kudumu  katika ustawi wa  watu binafsi, familia na jamii nchini Tanzania.


“Katika kuadhimisha Siku wa Miguu Iliyopinda duniani kwa mwaka huu na kama sehemu ya kujitoa kwetu kukuza ustawi wa jamii  tunatoa msaada wa shilingi milioni 110 kwa CCBRT  kwa ajili ya kusaidia matibabu ya  miguu iliyopinda katika hospitali yake. Msaada huu kwa matibabu ya miguu iliyopinda ni kielelezo kwamba Tigo   inaendelea kujikita katika kusaidia  utoaji wa huduma za afya katika CCBRT  na nchini kwa ujumla.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!