Monday, 5 June 2017

Alichoandika Mhe Freeman Mbowe kupitia ukurasa wake wa Instagram

Image may contain: 1 person
"Na kila wakati tulipokuwa tunapitia mazingira haya na muangalia Ndesamburo na uwezo wake najiuliza huyu mzee amekosa nini kwenye maisha yake unaangalia struggle anayoifanya Ndesamburo unawaangalia vijana wa Kitanzania wanacheza pool table, tunajiuliza kizazi chetu cha kesho kinafanya nini kuenzi kazi walizofanya wakina Ndesamburo wakina Mtei na wazee wengine wengi? 

Lakini ni dhahiri kutokana na hofu za watu kwamba leo tumejenga taifa lenye hofu, watu wamekuwa waoga kwa sababu viongozi wamependa kuingiza hofu katika jamii.

Ndugu zangu waombolezaji wazungu wanamsemo unaosema "The guilty are afraid" yani watu wenye hatia wana hofu.
Kwa hiyo kukosekana kwa uwakilishi wa serikli mahali hapa sio ajali ni hofu ya hatia, kwa heshima sana dada yangu Mbunge Mmasi pole na Ahsante kwa kufika Ahsante kwa ujasiri , Tunalia wote.
Nimeona vituko sana katika msiba wa Mzee wetu Ndesamburo alafu nikajiuliza mbona huyu Mzee ni mwema?
Labda niwaambie waombolezaji muelewe kwanza tuliamini kwa tukio hili la kihistoria ni vyema tukamsindikiza Mzee wetu kwa bendi ya polisi Brass Band ya polisi."

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!