ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Watanzania wote kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya gari juzi Jumamosi.
Bi Samia Suluhu akitoa salam za pole.
Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.
Amevitaka vyombo husika vihakikishe suala la usalama barabarani linapewa kipaumbele.
“Nawaasa madereva kuwa makini wawapo barabarani na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara,” alisema Bi Samia..
Aidha Bi Samia amemshukuru Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Katika ajali hiyo iliyotokea wilayani Karatu baada ya basi aina ya Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi wa Lucky Vincent Primary School wakielekea kwenye mtihani wa kujipima na wenzao kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo, jumla ya watu 35 waliaga dunia wakiwa ni wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja.
Serikali imesema italipia gharama zote za kusafirisha miili 35 ya waliofariki katika ajali ya hiyo.
Majeneza yenye miili ya marehemu yakishushwa kwenye gari na kupelekwa sehemu maalum kwa ajili ya kuagwa.
Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.
Majeneza yenye miili ya marehemu.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.
Bi. Samia akiwatia moyo wanafunzi wa Lucky Vincent.
Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.
Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.
Waombolezaji wakilia kwa uchungu.
Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.
Rais Magufuli kupitia ujumbe kwenye Twitter, ameelezea, jinsi alivyopatwa na huzuni kutokana na ajali hiyo.
“Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha. Tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu,”.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, akiongozana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati wa kuaga miili ya marehemu hao.
Sehemu ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika viunga vya Hospitali ya Mount Meru Arusha wakisubiri miili ya watoto hao kwa ajili ya kuagwa.
Waziri wa elimu wa Kenya Dkt Fred Matiang’i, mmoja wa wageni kutoka nje ya Tanzania waliohudhuria ibada hiyo, amewapa pole Watanzania kwa msiba huo.
“Kenya itaendelea kuwa pamoja nanyi kwenye kipindi hiki kizito cha msiba huu mzito uliowafika. Msiba huu si wa Tanzania peke yake ni wa wote hata kwetu Kenya Rais Kenyatta na mkewe wanawapa pole sana na kuwaombea,” alisema Matiang’i.
Bi. Samia akiwa mwenye masikitiko makubwa.
Kikosi cha Huduma ya Kwanza wakitoa msaada kwa waliopoteza fahamu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jinsia na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu akitoa salam za pole kwa wafiwa na Watanzania wote.
Wanafunzi wa Lucky Vincent wakionesha nyuso za huzuni wakati wa kuaga wenzao 32, walimu wao na dereva.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent.
No comments:
Post a Comment