Saturday, 6 May 2017

Habari kamili ya Wanafunzi 32 waliofariki Arusha.

Tanzania,Arusha
Image captionBasi la shule ya Lucky Vincent likiwa korongoni
Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha, takribani kilomita ishirini na tano kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ,kutoka Arusha hadi karatu ni km 150 na wanafunzi hao walikuwa wamebakiza kama km 5 ili kufika kule walikokuwa wanaelekea.


Karatu, Arusha
Image captionHarakati za uokozi zikiendelea
Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu iliyokuwa imebeba wanafunzi na waalimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano ,Mwandishi wa BBC mjini Arusha Ally Shemdoe, aliyeko mkoani humo, ni kwamba kutokana na mvua zinazoendelea kunyenya nchini Tanzania kwasasa, chanzo cha ajali hiyo kinadhanikuwa kuwa ugeni wa njia kwa dereva, utelezi na mwendo kasi na hivyo kusababisha basi hilo kutumbukia korongoni katika mto Malera.
Arusha
Image captionRaia wakiwa wamekusanyika katika shuleni hapo
Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda baina ya shule hizo mbili ikiwa ni utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa za kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, hii ni kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , kuwa maiti zilizopokelewa hospitalini hapo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu ni wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa ambapo wanafunzi wa kiume ni kumi na mmoja na wasichana kumi na nane ambapo inakamilish idadi hiyo ya maiti thelathini na wawili na majeruhi wawili na taarifa zinaeleza kwamba maiti zitahifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha , Fabian Dagalo amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye kuhusiana na msiba huo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!