Thursday, 11 May 2017
BUNGENI: Majaliwa aeleza hali ya sukari nchini kuelekea mwezi wa Ramadhan
Mbunge Jakuh Hashim Ayoub amemuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan na kuna tatizo la sukari huku wananchi wakihiwa na uhitaji na kwamba hivi sasa zipo tani 100,000.
Amemweleza Majaliwa kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.
Akijibu swali hilo Majaliwa amesema kuhusu kupungua kwa sukari na mahitaji yake nchini kuwa Serikali iko macho na itafanya jitihada za kupata mahitaji yote.
Amesema mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini nchini inazalishwa tani 320,000 hivyo mwaka huu imeagizwa sukari tani 80,000 na tayari tani 35,000 imeshaingia nchini.
Amewataka Watanzania kushirikiana kuwasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari waliyopandisha hivi sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Sidhani kama wafanyabiashara wanasikiliza watu zaidi ya kuangalia faida tu. Kupanda kwa bei ya sukari na vyakula vingine vinavyotumika kwa futari kama mihogo, viazi, ndizi na mahole ni tatizo lililopigiwa kelele kwa muda mrefu sana pasi na ufumbuzi. Nadhani jamii husika mfano kupitia councils kama BAKWATA na jumuiya nyingine za kiislamu zifikirie kuwa na ardhi na kulima vyakula hivyo lengo likiwa ni kuwasaidia watu hususan kwenye mfungo.
Post a Comment