Monday, 15 May 2017

Anayetuhumiwa kwa ujambazi auawa kwa kupigwa risasi Dar


Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.



Watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea leo (Jumapili) wamesema mtu huyo akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha kwenye gari kabla ya kuwekwa kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki moja iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini hapa.
Shuhuda wa tukio hilo, Leonard Macha amesema saa tatu asubuhi alisikia milio ya risasi eneo la jengo la Uhamiaji.
Macha ambaye ni mlinzi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lililo jirani na jengo hilo amesema polisi waliimarisha ulinzi eneo.
“Aliyekufa aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi walipiga risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi walipomfyatulia risasi na alikufa papo hapo,” anasema Macha.
Amesema wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema atazungumzia tukio hilo kesho atakapokutana na waandishi wa habari ofisini kwake

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!