Friday, 7 April 2017

Tanzania yapaa nafasi 22 Fifa

TANZANIA imepanda kwa nafasi 22 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘Fifa’ na sasa inashika nafasi ya 135 kutoka 157 mwezi uliopita.


Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya kufikisha pointi za jumla 218.
Kupanda huko ni ishara njema kwa kocha mpya wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Salum Mayanga aliyeanza kibarua hicho kwa ushindi katika mechi mbili za kalenda ya Fifa zilizochezwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mayanja amechukua nafasi ya Charles Mkwasa aliyejiuzulu. Katika mechi mbili zilizochezwa mwishoni mwa Machi, Stars iliifunga Botswana mabao 2-0 kabla ya kuifunga Burundi mabao 2-1.
Wakati ikicheza mechi hiyo, Botswana ilikuwa ya 116 na kutokana na kipigo hicho imeporomoka mpaka nafasi ya 120, na Burundi iliyokuwa nafasi ya 139 imeporomoka mpaka 141.
Katika nchi za zilizo ukanda wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Uganda iliyoshiriki fainali za Afcon Gabon Januari mwaka huu bado inaongoza kwa kushika nafasi ya 72 ikifuatiwa na Kenya 78, Rwanda ya 117 na Ethiopita ni ya 124.
Sudan na Sudan Kusini zimefungana katika nafasi ya 154 na Djibouti ni ya 194 huku Eritrea na Somalia zikifungana katika nafasi ya 206.
Kwa upande wa Afrika kwa ujumla Misri ndio inaongoza ikishika nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal nafasi ya 30 na Cameroon ni ya 33. Aidha kwa upande wa Dunia, Brazil imerejea nafasi ya kwanza baada ya kusubiri kwa miaka saba.
Tangu ilipoondolewa na Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 Afrika Kusini, Brazil imekuwa ikiongozwa na Hispania na Uholanzi waliokuwa wakishikilia nafasi ya kwana nza ya pili.
Ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Uruguay na Paraguay ulioifanya timu hiyo kukata tiketi ya kombe la dunia Urusi 2018 ndio umeibeba mpaka nafasi ya kwanza.
Timu zilizo kwenye kumi bora ya viwango hivyo nyuma ya Brazil ni Agentina, Ujerumani, Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!