Monday 3 April 2017

Mlemavu wa mikono aomba msaada

BAHATI Hemed (34), mlemavu ambaye hana mikono yote miwili anaomba msaada kwa Mtanzania yeyote anayeweza kumsaidia fedha za matumizi wakati atakapokuwa anasubiri na baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa uvimbe tumboni wiki ijayo katika Hospitali ya KCMC Moshi.


Akizungumza kwenye ofisi za Habarileo mjini hapa jana, akiwa safarini kwenda Hospitalini KCMC, Bahati ambaye huandika kwa kutumia mguu wake wa kushoto alisema anaomba msaada wa fedha kwa ajili ya matumizi yake na anayemsaidia, Taus Ramadhani (27) wakati atakapokuwa anasubiri na baada ya kufanyiwa upasuaji.
“Sina fedha yoyote kwa ajili ya kumlipa msindikizaji na mwangalizi wangu, Tausi na ninatakiwa kumlipa shilingi 250,000 kwa mwezi kutokana na huduma atakazozitoa wakati nikiwa hospitalini hapo,” alisema.
Akizungumza kwa uchungu, Bahati alisema hana fedha za matumizi na hivyo hajui yeye na msaidizi wake wataishi vipi, wapi na watakula nini wakati akisubiri kufanyiwa na baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Bahati alimshukuru Diwani wa Kata ya Cheyo, Tabora, Joseph Kitumbo kwa kutoa gharama za kufanyiwa upasuaji na majirani zake ambao wamechanga nauli ya kutoka Tabora hadi Moshi.
Aliomba msaada huo kutokana na ukweli kwamba hana mikono na hana uwezo wa kufanya kazi yoyote kutokana na kuumwa uvimbe huo tumboni, hivyo anaomba yeyote mwenye mapenzi mema amtumie fedha kupitia namba 0788955266 na 0757249557.
“Naomba Watanzania wanisaidie maana nateseka na uvimbe huu naomba wanisaidie nipate fedha za kutumia mimi na msaidizi wakati nikipata tiba ya matatizo haya ambayo yamegundulikwa mwaka 2011 katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete,” alisema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!