Friday, 7 April 2017

Jipatie Muongozo wa Kilimo bora cha Papai



 Leo napenda kukuletea habari njema kuhusiana na kilimo cha Papai. habari hiyo njema ni kuhusu Muongozo wa kulima kitaalamu (Master Plan). Master Plan (au Muongozo) ni huduma inayotolewa na mtandao Kilimo Biashara (www.kilimobiashara.netkwa ajili ya kumwezesha mkulima kulima kitaalamu hata pasipokua na mtaalamu, yaani akifuatilia muongozo huu anakua mtaalamu yeye mwenyewe. 


Hii inawasaidia sana wale ambao wanataka kufanya kilimo lakini hawajui kipi kianze na kipi kifuate.
Kutokana na uhaba wa wataalamu, wakulima wengi wamekua wanakosa ushauri wa kitaalamu na hii hupelekea wakulima wengi kupata hasara, kutokana na changamoto hiyo ndipo tulipokuja na wazo la kutengeneza Miongozo yenye utaalamu ambao mkulima yeyote anaweza kuielewa na kufuatilia vizuri. Miongozo hii ipo kwa lugha ya Kiswahili. Hapo awali tulianza kutengeneza Miongozo kwa ajili ya kilimo cha Nyanya, Tikiti, Vitunguu na Pilipili Hoho, ambayo imekua na muitikio mkubwa sana na kuwasaidia wakulima wengi. hata hivyo wakulima wengi walishauri tuendelee kutengeneza miongozo kwa mazao mengine, na maoja ya zao lililokua likiuliziwa kwa wingi ni Papai. Habari Njema ni kwamba Muongozo (Master Plan) huo wa kulima papai Kitaalamu umekamilika tayari.
Hapa chini nimekupa kionjo tu cha baadhi ya mambo utakayoyakuta kwenye Master Plan ya kilimo cha Papai.
Baadhi ya Yaliyomo kwenye Muongozo (Master Plan):
Uandaaji wa mashimo kitaalamu, na namna ya kutengeneza mchanganyiko mzuri wa udongo, mbolea, majani makavu na majivu.
Programu ya upigaji dawa za magonjwa na wadudu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hapa tumependekeza dawa zenye ufanisi mzuri kwenye kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbu kwenye mipapai. Wale wadudu weupe wasumbufu, ambao huweka utandao mweupe (Kitaalamu huitwa White mealybug), tumeweka dawa nzuri yenye kuwamaliza kabisa. Hivyohivyo kwa magonjwa na waududu wengine Muongozo huu unapendekeza dawa zake na namna ya kuzipiga
Programu ya Uwekaji Mbolea: kuanzia mbolea ya kupandia hadi mbolea za kuimarisha matunda kua na ngozi imara. Wakati gani wa kuweka mbolea hizo, na kiwango cha kuweka kwa mmea. Pia utajua namna ya kuchanganya mbolea mbili kwa uwiano mzuri wenye kuleta matokeo mazuri.
Programu ya Mbolea za majani (Booster): hapa utazifahamu mbolea zote za majani kuanzia za wakati mimea ni midogo hadi zile za kipindi cha matunda. Ili kuleta ufanisi zaidi tumeonyesha namna ya kuchanganya mbolea hizi za majani (boosters) na dawa za wadudu
Programu ya Umwagiliaji: Hapa utafahamu kiwango cha maji kinachohitajika kwenye kila hatua ya ukuaji ya mipapai. Pia utafahmu ni wakati gani wa kumwagilia kila siku, kila wiki na ratiba ya mwezi.
Shughuli nyingine zote muhimu zipo, na zimewkwa kwa mtiririko mzuri ambao kila mkulima ataelewa na kuweza kutekeleza ipasavyo.
Kwa wakulima watakaotumia Master Plan watapewa fursa ya kupata mafunzo na ushauri wa mara kwa mara kwa msimu mzima wa kwanza: (ushauri na mafunzo haya kuhsiana na papai yatatolewa bure kwa wale watakatumia huduma yetu hii ya Master plan)
Gharama ya Muongozo (Master Plan)
Kwa mwezi huu wa nne (April) Muongozo huo unapatikana kwa bei ya OFA ya 20,000 tu. Pia OFA hiyo itaambatana na kupatiwa Mchanganuo wa Gharama na FAIDA (Cost Benefit Analysis au CBA) kwa zao la Papai. Yaani ukilipa hiyo 20,000 unapatiwa Master Plan pamoja na CBA kama bonus. Baada ya muda wa ofa kuisha Muongozo huu utapatikana kwa gharama ya 50,000. Usikubali kupitwa na OFA hii,
Vigezo vya Ofa:
Muongozo huu na CBA vitatumwa kupitia email au whastapp,
• Malipo yatafanyika kwa njia ya mpesa kupitia namba yetu ya 0763 071007. Baada ya malipo utatuma email yako na Jina lako kwa ajili kutumiwa Muongozo huo. Hakikisha email unayotuma ni sahihi
• Email na jina utatuma kwa njia ya meseji (SMS) kwenye namba hiyohiyo uliyolipia. AU unaweza kutuma kupitia whatsapp.
• Ikiwa utapenda kutumiwa kupitia whatsapp, basi baada ya kufanya malipo utatutumia msg whatspp kupitia namba hiyohiyo (0763 071007)
Karibu sana
0763 071007
Email: ushauri@kilimobiashara.net
www.kilimobiashara.net

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!