TUNAOMBA RADHI KWA PICHA
Mkazi wa Kijiji cha Katambike Kata ya Ugala Wilaya ya Mpanda Njamili Kalatasi ambae ameshambuliwa na mnyama Chui wakati alipokuwa akiokoa ndawa wa Ng-ombe aliyekuwa amevamiwa na chui huyo Picha Na Walter Mguluchuma katavi yetu Blog
Na Walter Mguluchuma .
WATU wawili wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Katambike
kilichopo katika Kata ya Ugala katika wilayaya Mpanda mkoani Katavi
wamejeruhiwa vibaya na chui walipokuwa wakipambana nae baada ya
kiungia ndani ya zizi na kuwashambulia ng’ombe .
Wanandugu hao wametambuliwa kuwa ni pamoja na Maiko Joseph (27) na
Njamili Karatasi (22) .
Akizungumzia mkasa huo , Diwani wa Kata ya Ugala, Halawa Malendeja
alisema kuwa lilitokea juzi , saa kumi na mbili alfajiri ambapo
mnyama huyo aliingia kwenye zizi la ng’ombe nyumbani kwa Joseph Maiko
ambaye ni baba mzazi wa wawili hao waliojeruhiwa na chui huyo .
“Baada ya chui huyo kuingia zizini alimshambulia ndama wa ng’ombe
akiwa katika harakati ya kuondoka na ndama huyo ili akamle nje ya
zizi hilo …. Ndipo Njamila aliposikia purukushani hizo zilizomsukuma
atoe nje ya nyumba alimokuwa amelala na kwenda kwenye eneo la tukio
na kushuhudia chui huyo akitaka kutoka nje ya zizi hilo akiwa na
ndama huyo “ alieleza .
Aliongeza kuwa ndipo Njamili alipoingia zizini na kuanza kumshambulia
chui huyo kwa rungu … ndipo mnyama huyo alipomwachia ndama na
kuanza kumshambulia Njamili ambapo alipooona ameziwa alianza kupiga
mayowe akomba msaada .
Inadaiwa kuwa kaka yake Njamili aitwae maiko alimsikia mdogo wake
akipiga kelele akiomba msaada ndipo alipotoka nje ya nyumba alimolala
na kwenda kwenye eneo la tukio huku akiwa na ryngu mkononi .
“Maiko aliingia zizini na kuanza kumshambulia chui huyo kwa rungu
ili kumuokoa mdogo wake ….. mnyama huyo alimwacha mdogo wake akiwa
tayari amemjeruhi vibaya mkono wake wa kulia uliokuwa ukivuja damu
nyingi na kumrukia Maiko na kumuuma shavu lakulia na kumjeruhi
vibaya “ alieleza Malendeja.
Kwa mujibu wa Diwani huo , Maiko licha ya kung’atwa shavuni na mnyama
huyo alionesha ujasiri mkubwa kwa kuikamata miguu ya mbele ya
mnyama huyo na kuweza kumwangusha chini .
Diwani huyo aliongeza kuwa , Maiko akiendelea kupambana na mnyama
huyo huku , mdogo wake , Njamili aliendelea kupiga mayowe kwa kwa
nguvu zake zote ambapo majirani walipozisikia walikimbilia eneo la
tukio na kufanikiwa kumuua chui huyo .
Akizungumza akiwa amelazwa katika Hospitali ya Manispaa Mpanda,
Njamili alidai kuwa chui huyo alikuwa dume kwamba licha ya
kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake lakini alimjeruhi vibaya
mkono wake wa kulia .
Katavi yetu blog

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Simbo Raphael Kalinga alisema Halmashauri hiyo imepata taarifa za kutokea kwa tukio hilo na imetuma wataalamu wa idara ya wanyama pori kwenda kwenye Kijiji hicho..
Akizungumza akiwa amelazwa katika Hospitali ya Manispaa Mpanda,
Njamili alidai kuwa chui huyo alikuwa dume kwamba licha ya
kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake lakini alimjeruhi vibaya
mkono wake wa kulia .
No comments:
Post a Comment