Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa suluhisho la kumaliza mrundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani ni kuangalia aina ya makosa ya wanaostahili kuwekwa mahabusu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema suluhisho lingine ni kukamilisha uchunguzi haraka na kuwaachia huru waliobainika kutokuwa na hatia.
Nchemba amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Parole Bwalo la Maofisa Magereza Ukonga jana.
Amesema amewahi kuzungumza na mahabusu akagundua baadhi yao wamewekwa ndani kwa kesi ndogo ambazo zingeweza kumalizwa.
No comments:
Post a Comment