Saturday, 4 March 2017

Toka kwa Mdau: VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA

Image result for madawa ya kulevya


Wapendwa leo najitokeza hadharani mchana kweupe kuunga mkono kwa asilimia 100 juhudi zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya awamu ya tano kuhusu suala la madawa ya kulevya.



Hakuna asiyejua madhara ya madawa ya kulevya kwani tumeshuhudia jamii ikipata matatizo kutokana na baadhi ya watu kutumia au kujihusisha na madawa ya kulevya.
Kama nilivyowahi kuonya dhidi ya wanasiasa kutumia jambo au tatizo linalojitokeza katika jamii kama sehemu ya kujijenga kisiasa.Wapo ambao wamejitokeza kumshutumu bwana Makonda kuwa amefanya makosa kwa namna ya alivyoshughulikia suala hili.Kimsingi nadhani badala ya kumlaumu ni vyema kwanza akapongezwa kwanza kwa kuthubutu kufanya hilo alilolifanya maana katika historia huko nyuma tulishuhudia viongozi wengi wakishikwa na kigugumizi ama kwa woga wao. au kwa sababu orodha waliokabidhiwa yamo majina ya wanaowahusu labda Ndugu au rafiki au kuwa na hisa nao katika biashara wanazozijua wao.
Hili si suala ambalo nilitegemea litazua tofauti kubwa kiasi cha kuleta hata mfarakano Kati ya mihimili mikuu mitatu ya nchi yaani bunge mahakama na taasisi ya rais.Tofauti hizi ni kutokana na baadhi ya watu kwa namna moja au nyingine kutaka kulinda maslahi yao na ambayo yaweza kuwa ya kisiasa au katika hayo hayo madawa ya kulevya.
Nilitegemea kama taifa linalochukia madawa ya kulevya bila kujali itikadi za kisiasa.rangi.dini.cheo au kabila basi wote kama taifa kusimama imara bila kuyumba na kuunga mkono juhudi za kupiga vita madawa ya kulevya kwa kuwa si jambo jema kwa jamii.
Aidha badala ya kumshambulia mheshimiwa Paul Makonda kuwa amekosea.Nliichokiona mimi ni kuwa Paul Makonda hajakosea kuanzisha vita hii labda tuu utata no katika njia alizopitia ndizo pengine zina dosari kidogo na sheria zinazohusu mamlaka yake na hili ni labda linaweza kutokana na sheria kuweka mazingira magumu ya mamlaka mbambali katika kushughulikia madawa ya kulevya.Nionavyo mimi ingekuwa jambo la busara sana kwa suala kama hili linapojitokeza kusimama Kitu kimoja kama taifa kwa kuunganisha nguvu katika kupambana na madawa ya kulevya.Madawa ya kulevya ni jambo baya Dunia yote inalitambua hilo hivyo si vyema kuliacha liendelee.
Huko nyuma marehemu Amina Chifupa aliwahi kujaribu kulizungumzia kwa ukali kabisa tena kishujaa lakini alikutana na vipingamizi vikubwa sana.Kipindi hicho suala hili lililala kabisa na hivyo kutoa wanya kwa wahusika wa madawa ya kulevya kufanya walivyotaka na hata kufikia kuwa suala la kawaida kabisaa.Aidha hali hiyo ilidhihirisha jinsi taasisi zinazohusika na kupambana na dawa za kulevya kuwa kama likizo.Nampongeza muheshimiwa Makonda kwa juhudi zake za kumuenzi marehemu Amina Chifupa.Cha msingi kwa wale wanaokerwa na hatua alizochukua kwa kuona kuwa labda kwa namna moja au yingine kakosea kisheria katika mamlaka yake wasilumbane bali watoe ushauri wa namna bora ambayo inaweza kutumiwa ili mradi ushauri huo usiwe na lengo la kurudisha nyuma juhudi zilizoanzishwa.
Aidha nashauri serikali itizame upya sheria.sera na mifumo yake ili isaidie katika usimamiaji as utekelezaji wa mambo mbalimbali badala ya kuleta tofauti miongoni mwa wadau.
Suala la madawa si jukumu la taasisi ya kupambana na madawa tu peke yake ni pamoja na mamlaka zote za kiusalama na kinteligensia kwa kuwa taifa likiwa na watumiaji na wauzaji wa madawa ya kulevya haliko salama.
Aluta continua.....................


Kennedy Ernest Mchomvu Kirashy Jr.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!