Sunday, 5 March 2017

SABABU ZA MTOTO KUTOKUKUA KWA UWIANO SAHIHI


Image result for mtoto wa miezi sita
Watoto wanapofikia umri wa kuanza kwenda madarasa ya awali ndio ule wakati ambao mtoto hurefuka na mwili wake huwa na nguvu nyingi,huu ndio wakati ambao wanaanza kujifunza kujitegemea na kutengeneza wasifu binafsi(personalities).Mtoto huanza kubagua chakula,na kuamua anapenda au hapendi chakula kipi.


Watoto wanaobagua chakula huwa kwenye hatari kubwa ya kukosa virutubisho maalum vinavyoitajika kuwezesha ukuaji wao,kwani virutubisho hivyo huchangia ukuaji bora wa akili,mwili na hata hisia.
Ukuaji sahihi wa mifupa na meno kwa watoto umekua ni changamoto kubwa sana,kwani asilimia kubwa ya watoto hawapati vitamini muhimu,madini mwili na asidi mafuta ya kutosha kuwezesha ukuaji wao.
Asilimia kubwa sana ya watoto hawapati mboga na matunda yakutosha katika lishe zao.Watoto wenye ukosefu wa vitamin muhim,madini mwili,na aside mafuta za muhim (essential fatty acids) huwa na akili zilizozubaa na hawafanyi vizuri darasani na wana asili ya ukali,watoto wengine huwa na unene wa ziada ambao pia husababishwa na lishe mbaya,Lakini kubwa kabisa mtoto huyo hawezi kukua katika uwiano ulio sahihi.
Watoto wa mwaka mmoja adi mine(1-4)wanaitaji masaa 14 ya usingizi kila siku.wanatakiwa kupata usingizi wa mchana wa kati ya saa moja adi masaa matatu na nusu(1-3.5),usiku wanatakiwa kulala kati ya saa moja na saa tatu(1-3) na asubuhi waamke kati ya saa kumi na mbili na saa mbili (12-2) Ni kosa kabisa mtoto kua macho baada ya saa tatu,endapo mtoto wako huwa macho baada ya saa tatu ni kiashirio kwamba anashida au tatizo Fulani.
watoto wenye afya nzuri na wanaopata usingizi wakutosha huwa wenye furaha na nguvu.
Lishe mbaya kwa watoto husababiswa na ukosefu wa Elimu na ufaham mzuri wa vyakula na lishe bora wa wazazi,lakini kwa upande mwingine hali ya wazazi kutokujali watoto wao kwa sababu moja au nyingine pia huchangia tatizo hili.
Nini maana ya Lishe Bora(balanced diet)?ni lishe yenye virutubisho vyote kwa kiasi sahihi na uwiano sahihi ili kuwezesha afya bora.Virutubisho vyote sita lazima viwepo: wanga,protini, mafuta ,vitamin, madini mwili na maji.kwa ujumla hii ndio maana ya lishe bora,lakini wataalam wa afya husema lishe bora hutofautiana kati ya makundi mbalimbali ya binadam kutoka na uhitaji wa miili yao katika kipindi Fulani,wakimaanisha inayoweza kua lishe bora kwa mtoto mchanga haiwezi kua lishe bora kwa mtoto wa miaka kumi na mbili kwani miili yao inauhitaji tofauti.
Kwa mantiki hiyo basi ili lishe ya mtoto wa mwaka mmoja adi miaka minne iitwe lishe bora,ni lazima iwe na virutubisho vifuatavyo:
-wanga : ugali,wali,viazi,mkate
Mboga za majani na matunda kwa wingi-lenga kumpa mara tano kwa siku
-protini : nyama,samaki,mayai,maharagenjegere(angalao ale samaki mara mbili kwa wiki)
Baada ya kujua lishe bora ya mtoto,tuangalie umuhim na kazi za Virutubisho tulivyoainisha hapo juu.
Vitamini C
Mwili wa binadmu hauwezi kujitengenezea vitamin C,hivyo ni lazima ipatikane katika lishe.Vitamini C huwezesha utendaji bora wa akili,huusika katika kuendesha hisia,pia huuwezesha mwili kunyonya madini joto.
Vitamini A
hutengeneza Meno na Ngozi yenye afya nzuri na kufanya mtoto aone vizuri.inapatikana kwenye mayai,nyama,maziwa,cheese,karoti na mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea.
Vitamin D
huwezesha mwili kunyonya calcium,bila calcium mifupa haiwezi kukua katika uwiano sahihi wala kuwa na nguvu hivyo mtoto anaweza kupata matege na kua na mifupa dhaifu.Vitamini D nyingi hutoka kwenye mwanga wa jua,si lazima liwe jua kali.Ingawa vitamin D inapatikana pia kwenye Mayai na samaki wenye mafuta ni vyema kuhakikisha mtoto anatoka nje kucheza kila siku ilia pate mwanga wa jua ambao utampa vitamin D ya kutosha.
Madini Chuma(iron)
hutengeneza seli za damu,hasa seli nyekundu ambazo hutumika kusafirisha oxygen katika mwili wa mtoto. bila oxygen yakutosha mtoto hawezi kucheza,kama mtoto wako anachoka wakati wote kuna uwezekano mkubwa wa kua na upungufu wa madini joto.Madini joto hupatikana kwenye nyama,samaki,mbegu za maboga,brown bread,maharage na mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea.
Folate (asili ya familia ya vitamin B)
Huusika sana katika utengenezaji wa seli mpya,hutengeneza DNA,ni ya muhimu sana katika ukuaji wa vichanga na watoto wadogo.Folate inapatikana katika mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea,maharage,karanga ,korosho,hata ivyo spinachi ndio chanzo kikubwa kabisa cha folate.
Asidi mafuta Muhimu(Essential Fatty Acids-EFA’s)
Mwili hauwezi jitengenezea kirutubisho hiki,ni lazima kipatikane kwenye lishe,kuna familia mbili za EFA’s-Omega 3 na omega 6_ambazo zinaitajika kuwezesha utendaji mzuri wa ubongo,utendaji bora wa kinga za mwili,na kuwezesha afya ya akili kwa ujumla.hupatikana kwenye oily fish,na flax oil.Kama mtoto wako anashindwa kutulia darasani,anashindwa kukumbuka vitu,analala kwa shida au hapati usingizi vizuri basi kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kua na upungufu wa Omegas.
Calcium
Madini ya calcium ni kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno na pia inaendesha mfumo wa mapigo ya moyo na inasaidia damu kuganda kwa haraka.Bila vitamin D,mwili hauwezi nyonya calcium.calcium inapatikana kwenye mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea,karanga,maziwa ya Ng’ombe,na vyakula venye asili ya mbegu na katika maji(hard water)
Fibre(Nyuzi nyuzi)
Ni muhimu sana katika usagaji wa chakula mwilini.watoto wengi hupata shida kupata aja kubwa (constipation )kwa ajili ya ukosefu wa fibre katika lishe zao.ili kuepuka tatizo hili,hakikisha mtoto anapata fibre ya kutosha katika lishe yake.Matunda,mboga za majani,unga usiokobolewa na karanga ni vyanzo vizuri vya Fiber.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!