Rama Dee amesema hayo kupitia kipindi cha FNL cha EATV ambapo alizungumza moja kwa moja kwa njia ya skype akiwa nchini Australia kutokana na taarifa za msanii huyo kushikiliwa na polisi tangu Jumatano kwa tuhuma za kujihusisha na dawa ya kulevya.
Rama Dee amesema kwamba viongozi wanapaswa kuzingatia maneno wanayozungumza dhidi ya wasanii ili kuepuka kuharibu taswira za biashara za wasanii hao na heshima ambayo aametumia gharama kubwa na muda mrefu katika kuitengeneza kwa jamii.
Amempongeza Vanessa kwa kuitangaza nchi vizuri kimataifa na kusema kwamba anafanya kazi kubwa kuliko hata balozi.
"'Brand' ya Vanessa ni kubwa sana, ambayo nafikiri ameitangaza muda mrefu sana na siyo ndani tu hadi nje ya nchi ameitangaza Tanzania, yeye anafanya kazi zaidi kuliko hata balozi wa Tanzania, anatakiwa apewe pongezi. Sasa hivi mitandao ya nje inaandika tofauti kuhusiana na Vanessa,.Nina uhakika kama kiongozi lazima uwe na maono nikiongea hivi naweza kuathiri kitu gani kwa artist”. Alisema Rama Dee.
Katika hatua nyingine Rama Dee amempongeza Waziri Nape Nauye na kusema kuwa ameanza kufanya kazi yake vizuri, hivyo hata suala la wasanii anamuchia yeye ambaye ni Waziri mwenye dhamana kusimamia heshima za wasanii zisishushwe.
Katika mahijiano hayo, Rama Dee pia alipata fursa ya kufafanua kinachoendelea kati yake na director wa video Adam Juma.
No comments:
Post a Comment