Friday 31 March 2017

Mbunge wa Chadema afariki dunia



Mbunge wa Viti Maalum, Chadema Dk Elly Macha 
Mbunge wa Viti Maalum, Chadema Dk Elly Macha amefariki dunia leo nchini Uingereza.



Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha bunge, imesema kuwa Dk Macha alifariki akipata matibabu katka hospitali ya New Cross, Wolverhamton.
Dk Macha alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu bungeni kupitia Chadema.
Bunge limeahirisha vikao vya kamati vilivyokuwa vikiendelea leo hadi hapo kesho Aprili Mosi.
Tutaendelea kuwajuza zaidi kuhusu taarifa za kifo hiki.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!