Friday, 24 March 2017

Magufuli awaonya wanahabari Tanzania, asema 'hawana uhuru'


Dkt John Magufuli
Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionDkt John Magufuli amewaambia wamiliki wa vyombo vya habari wasifikiri "wana uhuru" wa kufanya watakavyo
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini humo kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.

Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.
"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe na mabalozi ikulu.
"Kwa ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."
Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu zilizotokea jana.
"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!