Maiti ya mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka 25-32 imeokolewa Jangwani baada ya kusombwa na maji. Maji hayo yametokana na mvua zilizonyesha Jijini Dar na kusababisha mafuriko.
Eneo la Jangwani limekuwa likiathiriwa na mafuriko mara kwa mara huku serikali ikifanya jitihada za kuwaamuru wakazi wa maeneo hayo kuhama bila mafanikio.
Boat inaandaliwa kuingizwa kwenye maji ili kuokoa watu
Hadi sasa mtu mmoja ameshaokolewa na Kikosi maalum cha uokoaji. wanatumia boat maalum inayojazwa upepo.
Mwili uliotolewa kwenye maji ni wa Kijana kati ya Miaka 25 na 32. Sina uhakika sababu hayupo hai.
Kikosi Maalum cha Uokoaji kikiendelea na kazi
=> Kwenye maji haya ya Msimbazi kuna watu bado wanaonekana vichwa kwa mbali. Hatujajua hali zao zikoje. Ila shughuli ya Uokoaji inaendelea.
=> Helicopter ya Polisi inaimalisha ulinzi kwa juu huku ikiangalia kama kuna watu zaidi wamekwama majini
Chopa ya Polisi
Kwa hali hii, bora mwaka huu Mvua isinyeshe Dar es Salaam Mwaka huu. Sababu leo Mvua ilinyesha kidogo tu lakini imeleta maafa. Je ikija kunyesha mvua kubwa itakuwaje?
Mungu atuepushie mbali balaa hili.
Naishauri Serikali kutumia mfano huu iwe fundisho kwao, Wazibue mitalo na sisi wananchi tuache kutupa vitu na uchafu kwenye mifereji ya maji.
PICHA KWA HISANI YA JMF
No comments:
Post a Comment