Thursday, 9 March 2017

Jela kwa zaidi ya miaka 5 kwa kuingiza heroin Uingereza kutoka Tanzania

[​IMG]
Adam Kamaizi Wimana baada ya kukamatwa na heroin Heathrow Airport

Mwanaume mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na miezi minne jela nchini Uingereza kwa kosa la kujaribu kuingiza nchini humo kilo 6.76 za heroin zenye dhamani ya Pounds 600,000 kutoka Tanzania.




Adam Kamaizi Wimana (46) ambaye ni raia wa Uingereza anayeishi Peel Court, Slough alikiri kosa lake. Pamoja na kifungo hicho, mahakama imetoa amri kwa Adam Kamaizi Wimana kutosafiri nje ya Uingereza kwa muda wa miaka miwili baada ya kumaliza kifungo chake.

Bw. Wimana (46), alikamatwa Januari 11, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow (Terminal 4) baada ya kutua na ndege kutokea Nairobi. Bw. Wimana alipanda ndege Nairobi baada ya kusafiri na mzigo huo akitokea Zanzibar, Tanzania.

Maafisa wa Heathrow walikagua moja ya mabegi yake na kungudua kuwa lilikuwa zito hata baada ya kutoa vitu vyote. Walipochunguza zaidi ndo wakakuta heroin imefichwa juu na chini ya begi hilo.

Vyanzo: 

1) Man jailed for trying to smuggle £600,000 of heroin

2) Heroin smuggler jailed after attempt to bring £600,000 worth of heroin into UK

3. Jail for drug smuggler caught at Heathrow Airport with £630k worth of heroin

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!