Friday, 20 January 2017

SERIKALI KUANGALIA UPYA KANUNI ZA TAFITI ILI ZIWEZE KUFANYA KAZI KWA WAKATI

 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.


 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Waziri Tizeba.
 Mkutano ukiendelea.
 Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kuhusu, Bioteknolojia ya kisasa katika sekta 
ya kilimo nchini.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa mada kuhusu utafiti wa mahindi yanayohimili ukame.
 Taarifa ikitolewa mbele ya Waziri Tizeba (kushoto)
 Safari ya kuelekea shamba la jaribio la mbegu za mahindi ikiendelea. Katikati ni Waziri Tizeba.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi kuhusu shamba hilo la jaribio hilo.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
 Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba  (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.

Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.

"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.

Alisema ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.

Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.

"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais  Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.

Alisema kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.

Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.

Akizugumzia kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya wananchi kuhusu matumizi ya  vyakula vya GMO alisema mitazamo hiyo inachochewa na wanaharakati kwa faida zao binafsi na kama wanaushahidi wa jambo hilo ni vizuri wakatoa ushahidi huo hadharani badala ya kupotosha umma.

"Kama mtu anaushahidi huo namuomba aniletee badala ya kuzungumza mitaani kwani wenzetu wa nchi zingine wanatumia vyakula hivyo na kama vingekuwa si sahihi wangewezaji kuvitumia" alihoji Tizeba.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk.Hassan Mshinda alisema kazi kubwa ya Costech ni kufadhili tafiti mbalimbali na kuhakikisha zinawafikia walengwa na akaishukuru serikali kwa hatua iliyofikia ya kuona taratibu na kanuni zilizopo jinsi zinavyorudisha nyuma maendeleo ya tafiti hizo za uzalishaji wa mbegu ambazo zikipatikana kwa wingi bei yake itakuwa ndogo tofauti na sasa na kumkomboa mkulima.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!