Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump, amewahi kuwa na ndoa mbili zilizovunjika kabla ya kumuoa, Melania ambaye ndiye first lady wa nchi hiyo.
Kutokana na ndoa hizo, Trump ana jumla ya watoto watano pamoja na wajukuu wanane. Ndoa zake mbili za mwanzo ziliishia kwa talaka zilizoandikwa sana kwenye vyombo vya habari za udaku.
Trump alianza kwa kumuoa mlimbwende wa Czech, Ivana Zelníčková, April 7, 1977. Walibahatika kupata watoto watatu, wa kiume, Donald Jr. (aliyezaliwa December 31, 1977), wa kike Ivanka (aliyezaliwa October 30, 1981), na wa kiume mwingine Eric (aliyezaliwa January 6, 1984).
Donald Jr., Ivanka, na Eric kwa sasa wanafanya kazi kama makamu wakuu wa rais wa kampuni ya Trump. Akiwa kwenye ndoa hiyo iliyokuwa imeanza kuparaganyika, Trump alianzisha uhusiano na muigizaji Marla Maples.
Mwaka 1990 Ivana na Trump walipeana talaka. Maples alikuja kuzaa mtoto wa kike, Tiffany na walikuja kufunga ndoa December 20, 1993.
Wawili hao walikuja kutengena May 1997 na talaka yao kukamilika June 1999.
Mwaka 1998, Trump alianzisha uhusiano na mlimbwende wa Slovenia, Melania Knauss, aliyekuja kuwa mke wake wa tatu.
Walifunga ndoa January 22, 2005. March 20, 2006, alipata mtoto wa kiume, Barron Trump.
Trump akiwa amemshika begani mtoto wake wa mwisho, Barron
No comments:
Post a Comment