Wednesday, 18 January 2017

Nigeria kuchangia wanajeshi 200 kwenda Gambia

Nigeria inachangia wanajeshi 200 kwa kikosi cha pamoja
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNigeria inachangia wanajeshi 200 kwa kikosi cha pamoja
Nigeria imethibitisha kuwa meli ya yake ya kivita inaelekea Gambia kama mazoezi wakati nchi za kanda zinajianda kuichukulia hatua za kijeshi Gambia.

Rais mteule Adama Barrow kwa saa yuko Senegal na anatarajiwa kuapishwa kesho, lakini Rais Yahya Jammeh anataka matokeo ya mwezi uliopita yafutwe na amekataa kuondoka madarakani.
Jana shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa mataifa ya magharibi mwa Afrika, yalikuwa yana andaa kikosi cha pamoja cha kuingilia kijeshi ikiwa Jammeh hataondoka madarakani.
Sasa shirika la habari la AP limemnukuu msemaji wa jeshi la wanamaji la Nigeria akisema kuwa jeshi la wanahewa la nchi yake linachangia wanajeshi 200 kwa kikosi hicho cha pamoja.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!