Tuesday, 17 January 2017

Mwanamke atumia mtandio kujinyonga


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Anastazia Francis miaka 48 amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa katika mtaa Nyasaka wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.




Taarifa ya jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imesema kuwa mnamo tarehe 16.01.2016 majira ya saa 11:00 asubuhi, mwanamke huyo alikutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba chake kwa kutumia mtandio ambao alikuwa ameuning’iniza kwenye dirisha juu.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo baada ya mumewe kuondoka alimtuma mwanae mkubwa aliyemaliza kidato cha nne aende dukani na mwingine mdogo mwenye umri wa miaka 06 aende kufagia na ndipo alipopata mwanya wa kwenda kujinyonga hadi kufa.
Tukio hilo lilijulikana baada ya mtoto wake mdogo kurudi ndani chumbani kuchukua shati na kumkuta mama yake akiwa amejining’inizi ndipo aliita watu ili waje kumsaidia.
Taarifa hiyo ya jeshi la polisi imesema kuwa upelelezi unaendelea ili kufahamu chanzo cha tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amewaasa wananchi pindi wanapopata matatizo waombe ushauri kwa watu wengine ili kuweza kuepusha maamuzi ambayo ni hatari katika maisha yao.

Kwa mtazamo wangu: Wanawake wengi wanateswa sana majumbani haswa vijijini, usikute huyu mama amepata matatizo lakini hakuweza kumwambia mtu yeyote, na hiyo ni tabia ya wanawake wengi, unapata matatizo unavumilia tu, mpaka inafikia wakati huwezi tena,na pia woga wa mwanaume,wengi wanatishiwa na hata kupigwa na waume zao, matokeo ndiyo kama hayo unaona bora nife kuliko mateso unayopata. we fikiria kama mama unafikia uamuzi wa kujiua na kuacha watoto wako, inasikitisha sana! Wanawake tusikubali kukaa namatatizo, nenda tafuta msaada, hata kwa jirani yako nenda.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!