Tuesday, 17 January 2017

Mbeya: Polisi Wafukua Jeneza la Aliyedaiwa Kufa na Kuzikwa, Baadaye Kukutwa Kitandani Amelala

mbeya-1
MBEYA: WAKAZI wa eneo la Isanga katika Jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa, mikasa na matukio ya vioja, baada ya mtoto HARUN JAILO KYANDO mwenye umri wa miaka 9 aliyedaiwa kufariki na mwili wake kuzikwa jana kwenye makaburi ya Isanga jijini humo ambapo baadaye alikutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya wazazi na ndugu kurejea kutoka makaburini.


mbeya-2
Wananchi wakiwa wamejaa makaburini kushuhudia tukio la kufukua jeneza hilo.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao akiwa amelala fofofo kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
mbeya-4
Jeneza mara baada ya kufukuliwa.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhiya leo kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makaburini hapo.
mbeya-3
Jeneza hilo likibebwa na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesimamia zoezi zima la kufukua jeneza hilo na baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo, kilichokutwa ni jeneza tupu likiwa halina kitu chochote.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!