DAR ES SALAAM: Maombi ya kufutiwa mashtaka yaliyowasilishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini hapa na Miriam Msuya, mke wa aliyekuwa bilionea mkubwa jijini Arusha, Erasto Msuya, leo yamesikilizwa na kutolewa uamuzi mdogo mbele ya hakimu Mwambapa aliyesema jamhuri ilikuwa na mamlaka ya kuiangalia hati ya mashtaka kabla haijaenda mahakamani hapo, hivyo jamhuri ikapewa siku mbili kuiangalia upya hati hiyo na hivyo kupangiwa Januari 11 mwaka huu kuwa siku ya kusikilizwa tena.
Utetezi huo uliwasilishwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, anayemtetea mteja wake, Miriam Msuya, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kudaiwa kumuua mdogo wa marehemu Msuya, Anethe Msuya, Mei 25, mwaka jana, Kigamboni jijini hapa.
Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Revocatus Muyela ambapo kupitia kwa wakili wao, Kibatala ameiomba mahakama iwafutie mashitaka hayo kwa kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu na haionyeshi kama walikuwa na nia ya kufanya uovu.
Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Anethe aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani Kibada. Wauaji hawakuchukua kitu chochote kwenye nyumba hiyo. Bilionea Msuya aliuawa Agosti, 2015 kwa kupigwa risasi. Cap: Miriam Msuya alipofikishwa mahakamani Kisutu leo.
GPL
No comments:
Post a Comment