Waakati akiwa hana chakula kwa ajili ya watoto wake, mwanamama Hellen wa nchini MArekani akaamua kwenda supermarket kwa ajili ya kuiba chakula kwa ajili ya watoto wake.
Alipofika, akaiba mayai matano ila akaonekana, hivyo polisi kuitwa na kuja kumkamata. Polisi yule kabla ya kumpeleka kituoni akamuuliza swali jepesi, umeiba nini?
Hellen huku akilia akamwambia kwamba aliiba mayai matano kwa ajili ya watoto wake wapate chakula. Alichokifanya polisi yule ni kumnunulia chakula kingi kwa ajili yake na watoto wake.
Hellen alilia sana, akamuuliza kwa nini alimfanyia hivyo na hakumpeka kituoni. Polisi akamjibu si wakati wote wa kuangalia sheria, wakati mwingine yatupasa kuonyesha ubinadamu.
No comments:
Post a Comment