Jeshi la polisi mkoani Dodoma, linawashikilia watu 3 ambao ni askari wanyamapori wa pori la akiba Swagaswaga wilayani Kondoa, wakituhumiwa kumuua mkazi wa kijiji cha Olimba wilaya ya Chemba kwa kumpiga risasi mgongoni wakimtuhumu kubeba nyama pori
Akizungumza ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 31, mwaka jana, saa 7:30 mchana katika kijiji cha Selya kata ya Selya wilayani humo.
“Marehemu ambaye hakufahamika jina lake lakini mkazi wa kijiji hicho, alikuwa akiendesha pikipiki huku akiwa amepakia kiroba kilichokuwa na sukari guru ndani yake, lakini askari wanyamapori hao walimuhisi amebeba nyama pori na bila kumsimamisha na kumhoji waliamua kutumia bunduki zao kumuua papo hapo,” alisema Mambosasa.
Mambosasa amesema baada ya kufanya mauaji hayo, askari hao waliubeba mwili huo kwenye gari walilokuwa nalo pamoja na pikipiki ya marehemu na kiroba cha sukari guru, kisha kwenda kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo la Swagaswaga.

Amesema baada ya kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo, walichukua pia pikipiki na kiroba na kuvificha kila kimoja mahali pake kwa lengo la kupoteza ushahidi wa tukio hilo.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa alisema wakati askari hao wanafanya tukio hilo, walishuhudiwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho ambaye alijificha porini ambaye aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Kondoa.
Akizungumzia tukio hilo kwa undani, Mambosasa alisema baada ya taarifa za msamaria mwema huyo, polisi walifuatilia na kuwakaata watuhumiwa hao ambao licha ya kuhojiwa walikana kuhusika na lolote lililodaiwa kufanywa.
“Vijana wetu wa upelelezi waliwabana sana, hali iliyowafanya wakubali na kuelezea tukio zima hadi walipouficha mwili wa marehemu, pikipiki na kiroba cha sukari guru,” alisema.
Kamanda huyo amesema katika eneo la tukio, askari wa upelelezi waliweza kugundua kipande cha sukari guru ambacho kilidaiwa ni sehemu ambayo alibeba marehemu ndani ya kiroba na kupakiza kwenye bodaboda.
Amesema tukio hilo ni la kizembe kufanywa na askari wanyamapori hao likiwa la pili kufanyika baada ya mwaka jana, askari mwingine kumuua raia kwa kumtuhumu kuhusika na kuua mnyama ndani ya pori hilo.
Aliwataja wahusika wa tukio hilo ambao wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ni George Grefee (26), Chini Paulo (40) na Christopher Waunko (36).
No comments:
Post a Comment