Thursday, 29 December 2016

Uingereza kufadhili kusambaza damu kwa njia ya ndege zisizo na rubani Tanzania

Ndege isiyo na rubaniImage copyrightDFID
Image captionNdege isiyo na rubani ikipaa
Uingereza itasaidia kufadhili matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani kusafirisha damu na vifaa vingine vya hospitali kwenye vituo vya afya nchini Tanzania.

Lengo ni kupunguza kwa kiasi kikubwa muda unaotumiwa kutuma akiba ya damu kwenye kliniki za afya katika mataifa ya Afrika kwa njia ya barabara na njia nyinginezo.
Mfumo utakaotumiwa utahusisha matumizi ya kamba ama uzio kuunganisha sehemu moja hadi nyingine, na mabonde hadi mabonde yenye makazi ya watu , mfumo sawa na ule umbao ulianza tayari kutumiwa nchini Rwanda mwezi October.
Wataalam wamepongeza mpango huo, lakini wanahoji kuwa ''ndege hizo za mizigo zisizokuwa na rubani (drones)'' kwa kutoweza kutumiwa na binadamu.
Shirirka la Uingereza la maendeleo ya kimataifa (Dfid) halijasema ni kiwango gani cha pesa litawekeza katika mradi huo nchini Tanzania na ni kwa muda gani .
Limetangaza mipango ya kufadhili majaribio ya ndege hizo nchini Nepal kuandaa ramani ya maeneo yanayotarajiwa kukabiliwa na hali mbaya ya hewa, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya maafa yanayoweza kutokea baadae.
"Uvumbuzi huu , ambao ni wa kisasa unahakikisha tunafikia matokeo bora kwa ajili ya watu masikini zaidi duniani na kutoa huduma bora na za thamini kutokana na pesa zinazotolewa na walipakodi Waingereza ,"alisifu katibu mkuu wa Shirika la maendeleo ya Kimataifa la Uingereza Priti Patel.
Ramani ya NepalImage copyrightDFID
Image captionDfid inaamini kuwa ndege zisizokuwa na rubani zinaweza kusaidia kuonyesha ramani za bara bara nchini Nepal ambazo zinaweza kusaidia kuonyesha njia za kuwasaidia watu katika maafa kama yale ya tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mwaka jana iwapo litatokea tena
Mfumo wa kamba wa ndege zisizokuwa na rubani (drones) - unaoitwa Zips - husafirisha ndege hizo kwa kutumia kwa kuziweka kwenye mbawa ndogo za ndege zinazofyatuliwa kutoka kwenye kifaa maalum na kwa kufuata mfumo ulioandaliwa awali kwa kutumia data za eneo.
Faida ya mfumo huo ni kwamba ndege inaweza kukabiliana na hali ya hewa ya upepo mkali kwa muda .
Kwa nadharia , ndege hizo zinaweza kupaa kwa takriban maili 180 ama kilomita 290 kabla ya kuishiwa nguvu za nishati .
Zip droneImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionAina hii ya ndege isiyokuwa na rubani inayofahamika kama Zip drone inaweza kubeba mzigo wa kilo moja na nusu
husafiri chini ya futi 500 kutoka ardhini ama mita 152 kuepuka anga ya juu inayotumiwa na ndege za abiria.
Tanzania, Rwanda na Malawi - ambazo zinatumia aina tofauti za ndege hizi zisizokuwa na rubani kwa usambazaji wa huduma za matibabu - zote zina sheria tofauti kuhusu utumiaji wa ndege zisizokuwa na rubani , suala ambalo lilizifanya kuwa mahala pema kwa majaribio ya aina hii.
Mapema mwaka huu, Tanzania pia iliidhinisha kisheria matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani katika Mbuga ya wanyama ya Tarangire kama sehemu ya juhudi za kuzuwia uwindaji haramu wa wanyamapori.
Dfid linakadiria kuwa usafirishaji damu na usambazaji wa huduma nyingine za afya kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kutoka nje ya mji mkuu wa Tanzania , Dodoma, kunaweza kuokoa $58,000 kwa mwaka ikilinganishwa na matumizi ya gari ama pikipiki kusambaza huduma hizo .
Lakini msemaji wa Dfid amesema kwamba kuokoa muda wa shughuli ya usambazaji wa huduma hizo ndio la muhimu zaidi.
"Safari za ndege hizo zinatarajiwa kuanza mapema mwaka 2017, na watakapofanya hivyo inakadiriwa kuwa mpango huo utasaidia katika uzazi salama wa watoto zaidi ya 50,000, ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa wanawake na watoto wachanga wanaosubiri kupata matibabu ya kunusuru maisha yao wa dakika 19 - utakaopungua kutoka dakika 110 ambao ndio unaotumiwa katika usafiri wa kawaida '' alibainisha.
Taasisi ya afya ya Ifakara -iliyobobea katika tiba za malaria, HIV, na kifua kikuu na matatizo ya afya ya akili- itakuwa ndio mshirika wa Dfid katika mpango huu .
Zip droneImage copyrightREUTERS
Image captionndege isiyokuwa na rubani aina ya Zip ikitua kwenye eneo salama
" Katika matumizi ya sasa ya ndege zisizokuwa na rubani , katika visa vya kipekee ambapo ndege zisizokuwa na rubani zinaweza kusaidia katika kuongeza ubora wa huduma za matibabu, mahitaji ya dhana ya huduma hii yanapaswa kupewa kipaumbele katika mahitaji ambayo mashirika ya kibinadamu yanakabiliana nayo," ilisema msemaji wa Dfid .
na kuongeza kuwa utafiti unahitajika kufanyika zaidi katika kutadhmini ikiwa mifumo inayotumiwa kwa sasa inafaa kama inavyodaiwa.
"Mashirika yanaonelea kuwa matumizi ya ndege za mizigo zisizokuwa na rubani yanahitaji takwimu kuhusu utendaji wake , saa zinazotumiwa kwa safari, viwango vya matatizo yake na takwimu nyinginezo za utendaji kazi wake"

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!