Thursday, 1 December 2016

TOKA KWA ZAMARADI!





zamaradimketemaAsiekupenda hawezi kuona UZURI wako
  • Asiekupenda atafumbia macho MAFANIKIO YAKO
    Asiekupenda hatataka kusikia HABARI NJEMA kutoka kwako
    Asiekupenda muda wote anatafuta KASORO ZAKO ili zimpe moyo 


  • Anachosahau kutokukupenda kwake yeye HAKUZIBI macho ya wengine kuona kilichomo kwako, wala HAKUSHUSHI thamani yako hata kidogo mbele ya wanaokupenda kiukweli, usije kuhangaika na wasiokupenda hata siku moja.. hawa wapo tu hawajaanza leo na wala hawataisha kesho na huenda wakaongezeka, kutaka kujisafisha mbele zao ni kupoteza muda na muelekeo wako wa maisha, Fanya unachokiona kwako sawa maana asiekupenda hakupendi tu hata ufanye nini.

    Usipelekeshwe Kifikra na watu wa aina hii, wana maumivu mengi, na LENGO LAO NI WEWE KUFELI, ni aina ya watu ambao hata wakushuhudie UNATEMBEA JUU YA BAHARI BILA KUZAMA WATASEMA UMESHINDWA KUOGELEA!! Inamana hawata concentrate na NGUVU YAKO inayokufanya utembee sehemu ambayo kila mtu ameshindwa kutembea na kutafuta ukawaida uliozoeleka ili tu wapatie pa kukutoa kasoro,
    ISHI MAISHA YAKO!!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!