Saturday, 3 December 2016

MREMBO ANNA NITWA AFANIKISHA UKARABATI WA CHOO CHA WODI YA KINAMAMA WANAJIFUNGUA WATOTO NJITI HOSPITALI YA DODOMA

 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.


Mrembo huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba 1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali ili kuweza kukarabati.

Aliendelea kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.

Kwa Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana. 

Kwa upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini hapo.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma 2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!