Tuesday, 20 December 2016

Mauaji ya balozi wa Urusi nchini Uturuki yahusishwa na ugaidi

Mshambulizi akipaza sauti na kuzungumzia Aleppo.
Image captionMshambulizi akipaza sauti na kuzungumzia Aleppo.
Urusi imeyahusisha mauaji ya Balozi Andrey Karlov na tukio la kigaidi.
Balozi huyo alipigwa risasi na mshambuliaji aliyekuwa akipaza sauti akitaja Aleppo

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow amesema Uturuki wamehakikishiwa kwamba kutakuwa na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na wote watakaokuwa wamehusika wataadhibiwa.
Meya wa Ankara amesema mauwaji hayo yamelenga huharibu mahusiano ya nchi hiyo na Urusi. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amesema Marekani iko tayari kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!