Saturday, 17 December 2016

Magufuli ateua mrithi wa Dk Mwele NIMR


Profesa Yunus Mgaya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Profesa Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).


Profesa Yunus Mgaya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Mwele Malecela ambaye uteuzi wake umetenguliwa jana usiku kutokana na kutoa taarifa za kuwapo ugonjwa wa zika nchini.
Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi wa Profesa Mgaya unaanza mara moja.
Profesa Mgaya alikuwa Mkugenzi Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kabla ya uteuzi wake kutenguliwa Mei mwaka huu.
Hata hivyo, baadaye Rais Magufuli alikutana naye katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumweleza yeye ni mtu mzuri na angempa kazi nyingine.

Mwananchi:

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!