Friday 9 December 2016

𝐃𝐀𝐖𝐀 𝐌𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝟏𝟎 𝐙𝐈𝐍𝐀𝐙𝐎𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐔.𝐓.𝐈



U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘𝓤𝓻𝓲𝓷𝓪𝓻𝔂 𝓽𝓻𝓪𝓬𝓽 𝓲𝓷𝓯𝓮𝓬𝓽𝓲𝓸𝓷𝓼’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.


Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra. Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.
Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.
𝐊𝐢𝐧𝐚𝐜𝐡𝐨𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐔.𝐓.𝐈:
=>Kisukari
=>Maumivu ya mishipa
=>Ajari katika uti wa mgongo
=>Ushoga (kwa wanaume)
=>Usafi duni
=>Upungufu wa maji mwilini
=>Kushikilia mkojo muda mrefu
=>Kurithi
=>Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.
𝐁𝐚𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐲𝐚 𝐝𝐚𝐥𝐢𝐥𝐢 𝐳𝐚 𝐤𝐚𝐰𝐚𝐢𝐝𝐚 𝐧𝐚 𝐳𝐢𝐬𝐢𝐳𝐨 𝐳𝐚 𝐤𝐚𝐰𝐚𝐢𝐝𝐚 𝐳𝐚 𝐔.𝐓.𝐈
=>Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
=>Kukojoa mara kwa mara
=>Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
=>Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
=>Mikojo kukutoka pasipo kutaka
=>Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
=>Kukojoa damu
=>Harufu nzito au mbaya ya mkojo
=>Homa
=>Kusikia baridi
=>Kutokujisikia vizuri
=>Kujisikia uchovu
Dawa mbadala 10 zinazotibu U.T.I
Chagua dawa 3 hata 4 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri zaidi na yanayodumu muda mrefu. Dawa namba 5 ni ya lazima.
𝟏. 𝐁𝐚𝐤𝐢𝐧𝐠 𝐒𝐨𝐝𝐚:
U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi. Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka.
Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.
𝟐. 𝐙𝐚𝐛𝐢𝐛𝐮 𝐧𝐲𝐞𝐮𝐬𝐢 (𝐁𝐥𝐮𝐞𝐛𝐞𝐫𝐫𝐢𝐞𝐬) 𝐧𝐚 𝐳𝐚𝐛𝐢𝐛𝐮 𝐧𝐲𝐞𝐤𝐮𝐧𝐝𝐮 (𝐜𝐫𝐚𝐧𝐛𝐞𝐫𝐫𝐢𝐞𝐬):
Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.
𝟑. 𝐍𝐚𝐧𝐚𝐬𝐢
Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’. Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.
𝟒. 𝐌𝐚𝐟𝐮𝐭𝐚 𝐲𝐚 𝐡𝐚𝐛𝐛𝐚𝐭 𝐬𝐨𝐝𝐚
Maambukizi na matatizo mengi kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo kwa ujumla yanatibika na mafuta ya habbat soda ikiwemo ugonjwa wa U.T.I unaowasumbua watu wengi miaka ya karibuni.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
𝟓. 𝐌𝐚𝐣𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐲𝐰𝐚
Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.
Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza hapa =>http://goo.gl/X9NHQY..
𝟔. 𝐕𝐢𝐭𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢 𝐂
Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini
Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo. Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge. Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.
𝟕. 𝐊𝐢𝐭𝐮𝐧𝐠𝐮𝐮 𝐬𝐰𝐚𝐮𝐦𝐮:
Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.
Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia; Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala kwa siku 7 mpaka 14.
𝟖. 𝐋𝐢𝐦𝐚𝐮/𝐧𝐝𝐢𝐦𝐮:
Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu. Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.
𝟗. 𝐔𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐣𝐚𝐧𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐥𝐨𝐧𝐠𝐞:
Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.
𝟏𝟎. 𝐌𝐬𝐡𝐮𝐛𝐢𝐫𝐢 (𝐀𝐥𝐨𝐞-𝐕𝐞𝐫𝐚):
Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa vinne, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona. Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.
Katika dawa hizi zote zilizojadiliwa hapa, napendekeza utumie dawa hizi kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kwa haraka, nazo ni; maji ya kunywa, kitunguu swaumu, limau, unga wa majani ya mlonge na mshubiri.
𝐕𝐈𝐓𝐔 𝐕𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐊𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐔𝐒𝐈𝐏𝐀𝐓𝐖𝐄 𝐍𝐀 𝐔.𝐓.𝐈
Huwezi kupona U.T.I au kuzuia U.T.I isijirudie bila kutimiza yafuatayo:
1. Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
2. Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
3. Penda kuwa msafi.
4. Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
5. Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.
6. Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda.
7. Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
8. Epuka kaffeina.
9. Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Dawa mbadala hizi 10 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.

Kwa Hisani Ya  fadhilipaulo.com


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!