Wednesday, 14 December 2016

Aliyetobolewa Macho Uso Kwa Uso na Scorpion Mahakamani



Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Ilala wakati shauri hilo lilipoletwa kwa ajili ya kusikilizwa.


Wakati mshitakiwa akipandishwa kizimbani alidai ana wakili wake hivyo mahakama ilisubiri kwa muda wakili wa mshitakiwa Juma Nassoro na baada ya kufika mahakamani ndio kesi ilianza kusikilizwa.
Kesi hiyo ina mashahidi sita na mpaka sasa ameshasikilizwa mmoja ambaye ni shahidi namba moja Said Mrisho ‘aliyetobolewa macho’ ambaye leo December 14 2016 ametoa ushahidi wake mahakamani hapo akielezea tukio alilofanyiwa.
Baada ya kusikiliza kesi, mahakama hiyo imeahirisha shauri hilo hadi December 28 mwaka huu ambapo itaendelea na shahidi wa pili.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!